Somabiblia Kila Siku 3Mfano
Leo tunaanza kusikia habari za mapigo yale kumi ya Mungu yaliyofanyika kabla Waisraeli hawajatoka Misri. Pigo la kwanza ni maji kugeuzwa kuwa damu, yaani Wamisri hawakuweza tena kuyanywa hayo maji (m.24). Lakini waganga wa Misri waliweza kuiga mwujiza huu (m.22)! Moyo wa Farao ulikuwa mgumu. Hakutaka wala hakuweza kumsikiliza Mungu. Mtu akiwa na moyo mgumu hawezi wala hataki kumsikiliza Mungu, hata akiona ajabu la Mungu. Neno la Mungu ndiyo silaha yetu kubwa ya kiroho! Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?(Mdo 2:37).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
SomaBiblia Kila Siku 3 ni mpango mzuri wa kukusaidia kusoma Biblia kwa njia rahisi. Ufafanuzi wa somo la kila siku unakupa mwanga na kiu ya kuendelea kulitafakari Neno la Mungu ukiwa peke yako au pamoja na wenzako.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz