Somabiblia Kila Siku 3Mfano
Pigo la sita ni majipu yaliyotumbuka. Haya yalikuja juu ya wanadamu na wanyama. Hayo majipu yenye kutumbuka yalisumbua sana. Mara kwa mara Farao alikuwa amefanya moyo wake kuwa mgumu, lakini sasa kuna tofauti: "Bwana akaufanya mgumu moyo wa Farao, asiwasikize" (m.12). Mtu kuchezea ukweli wa Mungu mara kwa mara, hali akitambua yote, ni tendo linaloleta hukumu ya Mungu. Mwishoni mtu huyu hawezi tena kumgeukia Mungu, kwa sababu Mungu anaepua nafasi ya kuungama dhambi. Isiwe mwisho wetu. Ombi: Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, unijaribu, uyajue mawazo yangu; uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, ukaniongoze katika njia ya milele (Zaburi 139:23-24).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
SomaBiblia Kila Siku 3 ni mpango mzuri wa kukusaidia kusoma Biblia kwa njia rahisi. Ufafanuzi wa somo la kila siku unakupa mwanga na kiu ya kuendelea kulitafakari Neno la Mungu ukiwa peke yako au pamoja na wenzako.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz