Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Bwana Yesu aja ([Bwana] apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote; 3:13)! Hivyo Wakristo waonywa wazidi kupendana. Hata mioyo yao wenyewe inawasukuma wafanye hivyo, maana Mungu amewapa Roho wake anayewafundisha (m.9f). Pia anawafanya kuwa si wazembe wala waombaji wanaowategemea wengine kwa mahitaji yao, bali wenyewe wafanye kazi kwa uaminifu na bidii kulingana na uwezo wao (m. 11f). Kwa njia hiyo watapata kuwa baraka kwa Wakristo wenzao na hata kwa "walio nje", yaani, wasioamini, maisha yao hayo yakiwavuta hao wampokee Yesu (m.12).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/