Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Wanaojitaabisha (m.12) usharikani kwa ajili ya waumini wenzao huonyesha wanavyowapenda. Walipiwe upendo kwa upendo, tukiwaheshimu kwa ajili ya kazi zao (m.13), si kwa ajili ya cheo kile au heshima ile tu. Tafakari tofauti iliyo kubwa kati ya kawaida ya ulimwengu huu na upendo wa Yesu uliomiminwa mioyoni mwetu kwa njia ya imani: Wavivu hufukuzwa; sisi tuwaonye kwa upendo. Wanyonge hukanyangwa na kutumiwa vibaya; sisi tuwatie moyo na nguvu. Adui hulipiwa maovu kwa maovu; sisi tuwabariki na kuwaombea (m.14; ling. Mt 5:44 ambapo Yesu anasema, Mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/