Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 5Mfano

Soma Biblia Kila Siku 5

SIKU 9 YA 31

Tukitaka kutimiza mapenzi ya Mungu kwetu (m.16-18), tuanze na kumshukuru Mungu kwa vipaji vyake. Hivyo tutashindwa kuacha kuomba, maana tutajaa furaha kwa ajili yake. Kama moto uzimikavyo, ukikosa hewa, Roho Mtakatifu hutuacha, akikosa mawasiliano kati yetu na Mungu, hapo Mungu akiongea nasi katika Biblia, nasi tukiongea naye kwa maombi (m.19). Unabii (m.20) si kutabiri mambo yajayo tu, lakini pia kuhubiri Neno la Mungu (Hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu; 2 Pet 1:20f). Tusiudharau, bali tuupime na tuushike kwa imani unabii ule upatanao na Biblia. Hivyo twaepuka uovu (m.22).

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 5

Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/