Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Wengi wahangaika, wakijitaabisha kwa kujenga maisha yao ya Kikristo. Lakini ni Mungu mwenyewe anayetutakasa (m.23). Basi tumwachie, maana yeye ni mwaminifu ambaye atuita, naye atafanya(m.24), tukikaa karibu naye kwa njia ya Neno lake na maombi. Kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu(1 Yoh 3:3). Busu takatifu (m.26) ambalo walibusiana shavuni pa uso wanaume kwa wanaume na wanawake kwa wanawake, lilikuwa alama ya kuwa Mungu amewaumba washarika kama familia katika Kristo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/