Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Bwana Yesu aja ([Bwana] apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote; 3:13)! Hivyo tuwe tayari kumlaki (4:17). Kuja kwake hugawa watu wote katika makundi mawili: 1. Wasioamini ni wa usiku, wamelala usingizi wa kiroho gizani. Hawamngoji Yesu, kwa hiyo kwao kuja kwake ni kama ajavyo mwizi. Hakika hawataokolewa (m.3). 2.Waumini ni wa mchana, hutoa nuru kwa imani na upendo wao. "Kuwa na kiasi" ni "kutokulewa" kama wasioamini. Ni "kuacha lolote lile litugeuzalo tulitazamie hilo badala ya Yesu". Tukikesha hivyo, tumaini litatulinda kama chapeo (m. 8) mpaka Yesu aje. Hakika tutaokolewa!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/