Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Bwana Yesu aja ([Bwana] apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote; 3:13)! Wakristo washike tumaini hilo, wakikabiliana na kifo. "Kulala" (m.13) hutumiwa na wengi badala ya "kufa", lakini kwa Wakristo lina maana maalum: Limejaa tumaini la ufufuo. Kama vile Yesu alivyofufuka, vivyo hivyo hao watafufuka, maana imani yao imewaunganisha naye, nao wamo katika Yesu (m. 14). Angalia upendo ulivyo mkuu kati yao hata ushinde mauti: Yesu (Bwana-arusi) mwenyewe (m.16) atakuja kuwachukua, nao waumini (Bibi-arusi) watamlaki (m.17), wakae pamoja milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/