Unayo Maombi!Mfano
“Tunalo la Kuomba!”
Msemo wa siku nyingi, “hana la kuomba” unaonyesha mtu ambaye anakabiliwa na hali ya kutoweza kabisa kufanikiwa. Au mtangazaji wa michezo anaweza kusema, “Aliomba,” pale ambapo mchezaji anapofunga goli dakika za mwisho tena akiwa mbali kabisa ya goli na filimbi ya mwisho kulia.
Lakini Mungu hakusudii kwamba maisha yetu ya maombi iwe ndio jambo la mwisho la kushinda magumu baada ya kujaribu njia na rasilimali nyingine. Ukweli ni kwamba Mungu anataka maombi yawe ni kiini cha maisha ya kila Mkristo: jambo la kwanza tunaloliendea tunapokuwa na mahitaji, na sio la mwisho. Anataka kusikia kutoka kwetu katika siku yote, kila siku, katika wakati tunapokuwa na mahitaji na katika wakati tuna kila kitu na kutoshelezwa. Pia Mungu anataka kuonyesha Upendo wake kwa njia nyingi kwa kuwa na mawasiliano ya kudumu na sisi tunapoomba.
Maombi ni ufunguo wa kuona mabadiliko chanya katika maisha na mazingira yetu, ni msingi wa kutufanya kukua katika mwendo wetu na Mungu.
“Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.” Yakobo 5:16
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Gundua kanuni ya kujenga maisha ya maombi yenye nguvu na ufanisi. Maombi – mawasiliano na Mungu kwa mtu binafsi – bi ufunguo wa kuona mabadiliko chanya katika maisha na mazingira yetu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)