Unayo Maombi!Mfano
“Funguo Sita za Maombi Yenye Afya na Yaliyo Sawa – Sehemu ya Kwanza”
1. Tambua unawasiliana na nani? “Baba Uliye mbinguni…”
Yesu alipowaagiza wanafunzi wake kumuomba Baba moja kwa moja, wazo hilo lilikuwa na uwezekano wa kukutana na maswali. Ukiangalia Agano la Kale lote, njia pekee kwa mtu wa kawaida ya kupeleka maombi yake kwa Mungu ilikuwa ni kupitia kwa kuhani. Ashukuriwe Mungu, Yesu alikuja kubadilisha hayo yote.
Kutokana na dhabihu iliyo kamili ya Yesu juu ya msalaba kubeba dhambi zetu, waamini sasa wana mawasiliano ya moja kwa moja na Baba. Ndio maana tunaomba kwa Baba wa Mbinguni “katika jina la Yesu.” Hata hivyo, hakuna kanuni katika kuomba, na kuomba maombi katika jina la Yesu ni sawa na kuomba moja kwa moja kwa Baba. Sehemu ya muhimu ya kukumbuka ni kwamba hakuna tena kizuizi cha mawasiliano kati yako na Mungu.
2. Tambua na kupeleka heshima na shukurani zako kwake kwa yote Aliyofanya kwa ajili yako. “…jina lako litukuzwe…”
Kwa kutenga sehemu ya maombi yako kulenga maalum katika kusifu na kumtukuza Mungu, unaondoa ile hali ya kujiangalia binafsi. Wakati Mungu anahitaji kusikia mahitaji na matakwa yetu, Anataka pia sisi kuonyesha shukurani kwa yote Aliyofanya na kutambua si “kuhusu sisi”. Ukweli ni kwamba, inahusu Yeye mwenyewe. Yeye ni Mungu wa upendo na utoshelevu, Mwenye kustahili sifa na utukufu. Unapoangalia juu ya Baraka ambazo Mungu amekupa wewe na neema ya ajabu ya kuwa na uhusiano Naye, utaona ni rahisi kumshukuru na kumtukuza. Pia utaona ni vigumu kuwa mbinafsi wa kujiangalia wewe mwenyewe tu.
3. Omba kwamba makusudi ya Mungu kwa Kanisa Lake na kwa maisha yako yatimizwe katika ukamilifu. “…ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko minguni.”
Maombi yenye uhai na ufanisi huja tunapoondoa mawazo yetu kutoka katika matatizo yetu ya nyuma na mambo mazuri ya baadae tunayoyatarajia. Kuendelea kukaa katika kukumbuka mambo ya zamani itakuzuia kwenda mbele. Chukua mtazamo wa Ki-Mungu, na usiruhusu changamoto au kushindwa kwa huko nyuma kutawala mawazo yako na kukuzuia kufikiri. Mwambie Mungu shauku yako ya kufikia uwezo wako mtimilifu katika Kristo, na muombe akusaidie kupanua maono na ndoto zako. Anataka wewe kufika mahali pa kusudi lako kamili katika maisha, na pia kwa Kanisa lake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Gundua kanuni ya kujenga maisha ya maombi yenye nguvu na ufanisi. Maombi – mawasiliano na Mungu kwa mtu binafsi – bi ufunguo wa kuona mabadiliko chanya katika maisha na mazingira yetu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)