Unayo Maombi!Mfano
“Maombi Binafsi”
Kuomba pamoja na rafiki, familia au hata kuomba kabla ya chakula ni njia nzuri ya kuwasiliana na Mungu katika mazingira ya kuonekana. Lakini zaidi ya kushiriki maombi ya pamoja, Mungu anatutaka tushiriki maombi ya mtu mmoja, yaani maombi binafsi pia – kati ya wewe na Mungu pekee yenu. Yesu ana haya ya kusema kuhusu faragha katika maombi yetu:
“Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako,usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.” Mathayo 6:6
Maelekezo ya Yesu kwetu ya kufunga mlango tunapoomba yanaonyesha kuwa Mungu anapendezwa na maombi binafsi katika maisha yetu. Hamu yake ni kuongeza uhusiano wetu binafsi na Yeye kupitia mawasiliano ya moja kwa moja ya mtu na Mungu. Mungu anaona kujitoa kwako katika kuwa na uhusiano Naye, na ameahidi kukubariki.
Mungu pia anatutaka sisi kuwa wazi na wakweli katika mawasiliano yetu na Yeye, kama vile tufanyavyo kwa watu tunaowapenda. Wakati kuomba kwa utaratibu neno kwa neno ni utaratibu wenye afya, ukweli ni kwamba Mungu anataka ile hali ya uhalisia tunapoomba Kwake na wala si mlolongo wa maneno ya kukariri ya sala. Yesu anasema hivi kuhusu ukweli na uhalisia katika maombi yetu:
“Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi (kurudia maneno kusiko maana). Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.” Mathayo 6:7-8
Ingawa Mungu tayari anajua tunayohitaji hata kabla hatujaomba, bado anatutaka sisi tujieleze Kwake kwa ukweli na matarajio kwamba Yeye anatuwazia mema. Anataka kujibu kila ombi kwa upendo na uaminifu.
Jambo lingine la muhimu kuhusu maombi binafsi ni kung’ang’ana na kutobadilika badilika. Mungu hachoki kusikia maombi yetu, hata kama ni yale yale tuliyokwisha peleka kwake. Yesu alisema hivi kuhusiana na bidii katika maombi yetu:
“Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.” Mathayo 7:7-8
Kutenga kila siku muda binafsi wa mawasiliano na Mungu ni muhimu katika kukua kwenye mwendo wetu wa Ukristo. Jaribu kuchagua muda kila siku ambao hautaingiliwa, na usijali kwamba Mungu atakuwa ameweka saa yake akiangalia muda gani unampa Yeye; Haangalii hilo. Yeye anakutaka wewe tu upatikane Kwake. Faragha, ukweli na kung’ang’ana ni sifa tatu muhimu ya maombi ya mtu na Mungu na itakusaidia wewe kujenga mahusiano ya karibu na Yeye. Utaufurahia muda huu wa thamani, na utafika mahali pa kumtegeme a Yeye katka jinsi ambayo hujawahi kufanya.
Kuhusu Mpango huu
Gundua kanuni ya kujenga maisha ya maombi yenye nguvu na ufanisi. Maombi – mawasiliano na Mungu kwa mtu binafsi – bi ufunguo wa kuona mabadiliko chanya katika maisha na mazingira yetu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)