Unayo Maombi!Mfano
“Mungu Anataka Kusikia kutoka Kwako”
Moja ya sababu ya maombi kuonekana kama jambo la mwisho pindi tunapokabiliwa na changamoto ni kwamba tunamwelewa Mungu visivyo. Wakati mwingine kwa makosa tunafikiria kwamba Mungu yuko mbali, akihusika na maisha yetu kwa umbali huo. Lakini ukweli ni kwamba, Mungu anahusika kwa karibu sana na maisha yako. Amekuumba wewe kwa furaha yake, na anataka kufanya kwa kupitia wewe na ndani yako!
Maombi yanaelezewa kwa urahisi kuwa ni mawasiliano na Mungu. Fikiria juu ya urafiki wa karibu ulionao. Hakika, mtu huyo rafiki atakuja kwako pindi unapomhitaji, tena huongea naye kila wakati, si ndivyo ilivyo? Unamshirikisha mambo yako, Naam, Mungu anataka uwe rafiki yake wa karibu. Uweze kumwambia kila kitu na cho chote, unaweza kucheka naye, unaweza kumwambia juu ya siku yako na Yeye, unaweza kuwa mkweli Kwake, unaweza kumshirikisha hamu za moyo wako. Jambo la msingi ni kwamba anataka kusikia kila kitu toka kwako! Mungu anataka sana muwe na mahusiano ya karibu nae, mawasiliano na Yeye.
“Tazama nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye,na yeye pamoja nami.” Ufunuo 3:20
Yesu anagonga katika mlango wa mioyo yetu, akitamani muda wa maana pamoja nasi wa ibada kwa mtu binafsi. Kufungua kwa urahisi huo mlango kwake Yesu agongaye kwa upole kwa ajili ya ibada ni mwanzo wa maisha ya maombi yenye mafanikio, ufanisi na matokeo na kujaa baraka za Mungu.
Mungu ndiye kimbilio la kweli katika maisha, na anataka kutuonyesha uaminifu na upendo - hakuna changamoto iliyo kubwa Kwake – Anataka tu kusikia kutoka kwako.
“Enyi watu, mtumainini siku zote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.” Zaburi 62:8
Kuhusu Mpango huu
Gundua kanuni ya kujenga maisha ya maombi yenye nguvu na ufanisi. Maombi – mawasiliano na Mungu kwa mtu binafsi – bi ufunguo wa kuona mabadiliko chanya katika maisha na mazingira yetu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)