Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Unayo Maombi!Mfano

Unayo Maombi!

SIKU 4 YA 6

“Mfano wa   Maombi Binafsi ya Ki-mungu Yenye Ufanisi”

Sala ya   Bwana ni moja ya maandiko ya Biblia yanayotambulika sana. Watu wengi   wanafahamu sala ya Bwana kwa kukariri, au wanaweza kuitambua mara   wanapoisikia. Yesu aliwaagiza wanafunzi wake: 

“Basi   ninyi salini hivi; ‘Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, Ufalme   wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo   riziki yetu, Utusamehe deni zetu, kama sisi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na   usitutie majaribuni, lakini utuokoe na Yule mwovu.’” Mathayo 6:9-13

Sala ya Bwana ni moja ya sala zinazoombwa sana hata   hivi leo. Lakini Yesu alipowapa maneno haya ya thamani wanafunzi wake,   Alikusudia iwe zaidi ya kutoa sala ya kukariri. Alitupa jinsi maalum ya kufanya   katika maombi yetu yote. 

Fikiria kwa muda juu ya mambo yanayokuzuia unapoomba,   au vizuizi gani vya maombi vinavyokukabili. Labda una tabia ya kujikumbuka   mwenyewe tu. Au huwezi kumaanisha wakati wa kuomba,  au unakatiza   maombi muda mfupi.  Haya ni matatizo ya   kawaida ambayo sote hukutana nayo mara kwa mara. 

Sala ya Bwana inatoa msingi wa kushinda hizo tabia na   vikwazo vinapogawanywa katika vipengele vianvoonekana katika sehemu zifuatazo.

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Unayo Maombi!

Gundua kanuni ya kujenga maisha ya maombi yenye nguvu na ufanisi. Maombi – mawasiliano na Mungu kwa mtu binafsi – bi ufunguo wa kuona mabadiliko chanya katika maisha na mazingira yetu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)

Mipango inayo husiana