Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mpe Mungu Nafasi ya KwanzaMfano

Mpe Mungu Nafasi ya Kwanza

SIKU 1 YA 5

“Mahali pa Mungu, Tunu Yangu!”

Nafasi ya Kwanza – tamanio la lengo la wote walio   katika mashindano. Iwe ni mashindano ya mtu mmoja au ni ya timu, aliyepata   alama nzuri za magoli au muda ndiye huwa mshindi, na siku zote nafasi ya   kwanza ndiyo yenye tuzo ya juu kwa huyo aliyefanikiwa kufikia kiwango hicho   cha utendaji. Siku zote ndivyo ilivyo, isipokuwa kwa jambo moja lisilo kawaida. 

Kabla hatujaokolewa, huwa tunachukua nafasi ya kwanza   katika maisha yetu  – tunaishi kwa   ubinafsi, tukitimiza shauku zetu binafsi, tukiendeleza mambo yetu. Lakini   pindi tunapokuwa Wakristo, nafasi ya kwanza si yetu wenyewe tena kuikalia, ni   mali ya Mungu. 

Kumpa Mungu nafasi ya kwanza huanza katika ile siku ya   kuokolewa, lakini kumruhusu Mungu kubakia wa kwanza katika maeneo yote ya   maisha yetu ni jambo linaloendelea. Tunapofanya hivyo, tunaishi maisha yenye   utoshelevu na kubarikiwa katika Kristo hapa duniani, na kurithi uzima wa   milele wa Baraka isiyoneneka pamoja na Mungu milele Mbinguni.

"Kila mmoja anayeshindana katika michezo huingia   katika mazoezi kwa nidhamu kubwa. Hufanya hivyo ili kupata tuzo isiyodumu,   lakini sisi twafanya hivyo kwa ajili ya tuzo inayodumu milele. I Wakorintho 9:25

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Mpe Mungu Nafasi ya Kwanza

Kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yetu si tukio la mara moja . . .ni mchakato wa maisha kwa kila Mkristo. Uwe ni Mkristo mpya au mfuasi wa Kristo “wa miaka mingi”, utagundua kuwa mpango huu ni rahisi ku - uelewa na ku - utumia, na ya kuwa ni mkakati wenye ufanisi wa hali ya juu kwa maisha ya ushindi ya Kikristo.

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)

Mipango inayo husiana