Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mpe Mungu Nafasi ya KwanzaMfano

Mpe Mungu Nafasi ya Kwanza

SIKU 2 YA 5

"Mungu   Amekupa Wewe Nafasi ya Kwanza Moyoni   Mwake”

Utafikiria   nini kama mtu akikuambia kwamba Mungu anakuona wewe kama mtu ambaye hukuwahi   kutenda dhambi? Ukweli ni kwamba, kwa sababu ya kazi ya ukombozi ya Yesu   Kristo pale msalabani, hivyo ndivyo Mungu akuonavyo. Kama Wakristo,   tumesamehewa, tumeoshwa, na tu huru! 

Hii   inamaanisha kuwa wewe ni mtakatifu: mtu aliyefanywa mwenye haki katika   Kristo. Wewe ni mkamilifu, mtakatifu na asiye na waa katika macho ya Mungu. Anakuita   wewe mwana Wake, mrithi wa utajiri wake, na rafiki Yake. 

"Bali   ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya   Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie   katika nuru yake ya ajabu." I Petro 2:9

Kuelewa   kwa usahihi jinsi Mungu anavyotuona inaanzia na jinsi sisi tunavyomuona   Mungu. Mungu haangalii kwa kutoka mbali akitusubiri sisi kufanya makosa ili   atuadhibu. Huu ndio  ukweli. 

Angalia   mstari huu unasema nini: 

"Bali   wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale   waliaminio jina lake,  - waliozaliwa,   si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali   kwa Mungu." Yohana 1:12-13

Mungu   humuona kila mmoja wetu kama mtoto Wake wa thamani. Yeye ni Baba mpendwa   anayetupa kibali na kutujali kwa huruma zake zisizo na kikomo. Baadhi ya   maandiko katika Wimbo Ulio Bora yanaonyesha huo upendo wa ajabu wa Mungu   kwetu kwa kulinganisha na upendo wa mume na mke. Waebrania 11:6 inatuambia   kwamba Mungu huwapa thawabu wale wamtafutao. 

Mungu   humuona kila mmoja wa watoto Wake katika njia tofauti kabisa ya jinsi sisi   tunavyojiona. Kuelewa jinsi Mungu amuonavyo kila mmoja wetu huonekana katika   kazi ambayo Kristo huanza katika maisha yetu mara tu tunapopokea wokovu. 

"Hata   imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita   tazama! Yamekuwa mapya." II Wakorintho 5:17

"Yeye   asiyejua dhambi alimfanya dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya   Mungu katika Yeye." II Wakorintho 5:21

Kufanywa   kiumbe kipya ni kazi ya kiungu ya Mungu; kubadilishwa kabisa kwa hali yetu ya   kiroho na utu wa ndani. Ametusamehe kabisa na kutusafisha kutoka dhambi zetu   – za zamani, sasa na baadae. Sasa tuna mahusiano sahihi na Yeye.

"…Kama   mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali   nasi." Zaburi 103: 12

Tu watu wa   Mungu tusio na waa lolote la dhambi;walio wenye haki Wake kupitia kazi   aliyofanya Yesu msalabani. Hakika Mungu ametupa nafasi ya kwanza moyoni Mwake!

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Mpe Mungu Nafasi ya Kwanza

Kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yetu si tukio la mara moja . . .ni mchakato wa maisha kwa kila Mkristo. Uwe ni Mkristo mpya au mfuasi wa Kristo “wa miaka mingi”, utagundua kuwa mpango huu ni rahisi ku - uelewa na ku - utumia, na ya kuwa ni mkakati wenye ufanisi wa hali ya juu kwa maisha ya ushindi ya Kikristo.

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)

Mipango inayo husiana