Mpe Mungu Nafasi ya KwanzaMfano
“Kushinda Mapambano ya Maisha kwa Msaada wa Mungu”
Kuna mapambano ya maisha siku zote yanayokabili maisha yetu. Upande mmoja ni mashinikizo asili ya zamani ya dhambi – zile tabia za zamani, tamaa na dhambi ambazo zimekuwa vigumu kwetu kuzishinda. Muda unavyoendelea tunavyozidi kukomaa katika mwendo wetu na Mungu, shinikizo la asili ya dhambi hupungua nguvu. Upande mwingine ni kukua kwa utawala wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Hizi ni nguvu mbili zinazopingana kama inavyobainishwa katika Wagalatia:
“Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.” Wagalatia 5:16-17
Neno la Mungu linatuhamasisha sisi “kuishi kwa Roho.” Kwa maneno mengine, ni lazima turuhusu umiliki wa Roho Mtakatifu ili kushinda juu ya mashinikizo ya asili ya dhambi katika mkaisha yetu.
Mara nyingi, hili ni rahisi kusema kuliko kulitenda. Asili yetu ya dhambi hutusukuma kufanya uamuzi kutosheleza shauku zetu zenye ubinafsi. Hii huitwa kujaribiwa, na Yakobo analielezea namna hii:
“Mtu ajaribiwapo, asiseme Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja wetu hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.” Yakobo 1:13-14
Ni mpaka pale uamuzi unapofanyika kwa upande wetu wa kujiachia kuingia katika tamaa ndipo huko kujaribiwa hugeuka kuwa dhambi.
“Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.” Yakobo 1:15
La kushangaza, ikiwa ni sehemu ya upendo wa Mungu usioelezeka na neema yake kwa Wakristo wote, Mungu hutusamehe na kutusafisha kutoka katika dhambi zetu zote. Sisi tumesamehewa kabisa kwa 100% .
“Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” I Yohana 1:9
Lakini bado iko hatari ya kutojilinda na dhambi. Pamoja na kwamba Mungu anatusamehe na kutuosha, hafuti ile njia ya uharibifu na mazingira ambayo matokeo ya dhambi huacha nyuma. Wakati ambapo Mungu hutusaidia katika wakati mgumu, hata kama ni maamuzi yetu sisi wenyewe ndio yaliyosababisha, njia bora ya maamuzi kwetu ni kujizuia kufanya maamuzi yaletayo dhambi.
I Wakorintho inaelezea mambo mawili muhimu ya kushughulika kwa ufanisi juu ya tamaa na dhambi:
“ Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.” I Wakorintho 10:13
Kwanza ujue kwamba hauko peke yako katika hayo mapambano. Ufahamu kuwa Wakristo wenzako nao wanapitia hayo, aidha iwe ni siku 30 au miaka 30 ya kutembea kwao na Mungu, bado wanapambana na dhambi na majaribu kama unayokabiliana nayo wewe.
Pili, ni kwamba Mungu hataruhusu tujaribiwe hata kufika mahali ambapo hatuwezi kufanya uamuzi wa kushinda dhambi. Wakati wote atatufanyia njia ya kushinda. Kazi yetu, hata ikiwa ngumu kiasi gani, ni kupata njia ya kutoka katikati ya majaribu yanayotukabili.
Sehemu inayofuatia inatoa mkakati wa Ki-Biblia wa kushughulikia dhambi na majaribu kwa ufanisi. Kuutumia mpango huu ni njia moja zaidi ya kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yako!
Kuhusu Mpango huu
Kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yetu si tukio la mara moja . . .ni mchakato wa maisha kwa kila Mkristo. Uwe ni Mkristo mpya au mfuasi wa Kristo “wa miaka mingi”, utagundua kuwa mpango huu ni rahisi ku - uelewa na ku - utumia, na ya kuwa ni mkakati wenye ufanisi wa hali ya juu kwa maisha ya ushindi ya Kikristo.
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)