Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mpe Mungu Nafasi ya KwanzaMfano

Mpe Mungu Nafasi ya Kwanza

SIKU 3 YA 5

“Mungu   Anataka Nafasi ya Kwanza Moyoni Mwako”

Katika   jamii ya leo, wengi huweka uthamani wao katika utajiri, wako juu kiasi gani   katika kazi, jinsi gani wamefanikiwa kibiashara au wanamjua au kujulikana na   nani? 

Lakini   ikiwa mtazamo wetu juu ya umuhimu unasimamia mambo haya, tutajisikia vizuri   tu pale tutakapofanikiwa katika maeneo hayo. Utajiri wetu na mafanikio   vitakapoporomoka, kujithamini kwetu nako pia kutashuka kwa kuwa msingi wetu   si thabiti. Yesu anaelezea hili kama ifuatavyo: 

“Lakini   yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya   ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na   maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa.” Luka 6:49

Utambulisho   wetu unaendana na msingi tunaoweka juu yake. Kwa kuweka utambulisho wetu juu   ya msingi wa mwamba imara Yesu Kristo, hali yetu ya utoshelevu katika maisha   haitategemea hali inayobadilika ya vitu vya muda mfupi. 

Kriso   anapokuwa msingi wetu, uthabiti wetu  ni   kama huu: 

“Mfano   wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya   mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze   kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.” Luka 6:48

Fikiria   kwa muda juu ya uchaguzi mwingi wa maamuzi unaokuwa nao katika maisha kujenga   msingi wa maana. Hii inaweza kuhusisha mali, kazi, mwonekano, familia, nguvu   au mtu unayemjua. Je kuna mengine unayoweza kuyafikiria? Juu ya vitu vyote   tunavyoweza kuweka utambulisho wetu kwavyo, ni Yesu pekee ndiye   anayetuhahakishia maisha ya ushindi ya Kikristo.

Lakini   ukichunguza uchaguzi mwingine, hakuna ulio mbaya au uliojaa uovu. Uhalisia ni kwamba, mara nyingi, kuna   maeneo mengi muhimu ya wajibu ambayo Mungu ametupa katika maisha yetu. Lakini   katika kitabu cha Mathayo, Yesu anatusaidia kufahamu la kufanya. 

“Kwa   sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini;   wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na   mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala   hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao.   Ninyi je! Si bora kupita hao?” Mathayo 6:25-26

Tunapogundua ukweli huu katika maisha yetu binafsi, tunapata   amani na utoshelevu, na kuwa huru kutoka katika hofu na mashaka. Hali hii   inafikiwa tunapomweka Yesu kuwa nambari moja katika maeneo yote ya maisha   yetu. 

“Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na   hayo yote mtazidishiwa.” Mathayo   6:33

Sisi wote   tuna ndoto, malengo na matamanio  kwa   kuwa ametuumba hivyo. Lakini kumweka Yesu kwanza hukufanya uchunguze   vipaumbele na matamanio kwamba kwa nini utamani kufanya au kupata mambo   unayotaka. Anapokuwa ni wa kwanza katika ndoto na matamanio yako, maisha yako   yatajaa furaha na ukuu!

Mungu   anapoleta jambo linalotatiza moyo wako, mwitikio wako muhimu unapaswa kuwa   aliye tayari kufanya mabadiliko. Mabadiliko yanaweza kuwa kitu kigumu wakati   mweingine, lakini siku zote Mungu anatuwazia jambo linalofaa, na anataka wewe ukue kiroho. 

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Mpe Mungu Nafasi ya Kwanza

Kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yetu si tukio la mara moja . . .ni mchakato wa maisha kwa kila Mkristo. Uwe ni Mkristo mpya au mfuasi wa Kristo “wa miaka mingi”, utagundua kuwa mpango huu ni rahisi ku - uelewa na ku - utumia, na ya kuwa ni mkakati wenye ufanisi wa hali ya juu kwa maisha ya ushindi ya Kikristo.

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)

Mipango inayo husiana