Mpe Mungu Nafasi ya KwanzaMfano
“Pointi Tano za Mkakati wa Kuishi Katika Ushindi”.
Sehemu hii inatoa pointi 5 za mkakati wa Kibiblia wa kushughulika kwa ufanisi na dhambi na majaribu. Kuutumia mpango huu ni njia moja zaidi ya kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yako!
1. FAHAMU KWAMBA MUNGU ANAKUONA WEWE KUWA NI MTU MKAMILIFU, MTAKATIFU NA ASIYE NA WAA, kupitia kazi ya Yesu Kristo. (Soma II Wakorintho 5:21.) Mara nyingi hukumu na aibu ni matokeo mabaya ya dhambi yanayoharibu. Kufahamu kuwa hakuna hukumu ya makosa kwao walio katika Kristo Yesu, bila kujali dhambi ni jambo la msingi kwa maisha ya ushindi (Warumi 8:1).
2. KIRI DHAMBI ZAKO. (Soma I Yohana 1:9.) Kukiri dhambi zetu ina maana ya kuzikubali kwanza hizo dhambi katika mioyo na akili zetu, na baadae kuzikiri mbele za Mungu. Kukiri dhambi zetu si lazima kwamba zifahamike na watu. Kukiri ni kati yako wewe na Mungu.
3. WAJIBIKA. (Soma Yakobo 5:16.) Kutafuta rafiki wa karibu, mkristo anayeweza kutumainiwa, mchungaji au mwana familia ambaye atakuwa msiri wako ni njia yenye ufanisi ya kuleta uwajibikaji na msaada wa maombi katika mapambano.
4. JIEPUSHE NA VYANZO VYA MAJARIBU. (Soma Yakobo 1:13-15.) Hii ni pointi yenye changamioto zaidi katika utekelezaji , na inahitaji ubunifu wa mawazo na mipango. Ukweli ni kwamba kama utaweza kujiepusha na jaribu, utazuia dhambi.
5. SOMA NENO LA MUNGU. (Soma Zaburi 119:11.) Neno la Mungu linatuambia wazi kuwa “tunapoliweka mioyoni mwetu,” lenyewe hutupa nguvu maalum ya kusema hapana kwa majaribu ya tamaa na dhambi.
Kuhusu Mpango huu
Kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yetu si tukio la mara moja . . .ni mchakato wa maisha kwa kila Mkristo. Uwe ni Mkristo mpya au mfuasi wa Kristo “wa miaka mingi”, utagundua kuwa mpango huu ni rahisi ku - uelewa na ku - utumia, na ya kuwa ni mkakati wenye ufanisi wa hali ya juu kwa maisha ya ushindi ya Kikristo.
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)