Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi!Mfano
“Sheria ya Dhahabu”
Iwe ni mwanasiasa, mfanyabiashara, mnenaji wa makongamano, au hata mtu wa kawaida, watu kutoka kila aina ya maisha mara kadhaa hurejea wema wa Sheria ya Dhahabu. Ukweli ni kwamba, kila mtu alishaisikia na anajua maana yake.
Watu wengi watakubali kuwa “kuwafanyia wengine kama ambavyo tungejifanyia sisi” ni jambo la muhimu katika jamii. Katika maeneo mengi, ni utaratibu unaobeba utamaduni wa watu, familia na urafiki pamoja. Sheria ya Dhahabu inaonyesha sifa ya kuwatumikia wengine, kuonyesha ukarimu na kuwasaidia wao walio katika uhitaji.
Yesu alikuwa ni mwanzilishi wa Sheria ya Dhahabu, ambayo ni moja ya vipaumbele muhimu vya maisha ya Kikristo yaliyofanikiwa.
Kama Wakristo, Mungu amemuita kila mmoja wetu kuikuza imani yake katika kiwango cha kuwa si watu wanaoamini juu ya Mungu tu. Shauku yake ni kila mmoja wetu kuweka imani yake katika matendo kwa kugusa maisha ya wengine, kwamba tumtukuze Mungu kwa kuonyesha upendo na neema Yake kwao.Hii ndio kuishi kwa kweli kwa Sheria ya Dhahabu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Maisha yenye kusudi na yaliyojaa furaha, hujengwa kwenye mahusiano, upendo na imani. Kama unataka njia iliyonyooka zaidi ya mpango wa Mungu kwa maisha yako, tumia mpango huu kukusaidia kuweka mkazo katika hilo lengo lako. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2