Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi!Mfano
“Tumikia Wengine”
Maana ya kutumika ni kule kupatikana katika kufikia hitaji la mtu fulani. Kufikia huko kunaweza kuhitaji muda wetu, kipawa chetu, rasilimali na juhudi zetu; lakini kutumika katika upendo kwa Mungu na kwa wengine yaweza kuwa moja ya uzoefu wa maisha wenye furaha kuu na unaoleta ijara.
Kuitikia mahitaji ya wengine kunaweza kuja katika njia nyingi na mkazo unaweza kuwa kwa Wakristo na wasioamini kwa pamoja. Siku zote kuna fursa ya kutumika katika kanisa la mahali kwa mtu mmoja au kama sehemu ya timu. Una kitu fulani cha ajabu cha kutoa!
Pia kuna fursa zinazojitokeza katika mtu mmoja mmoja unapokutana na watu, au kuhusika na hitaji la mtu fulani, na kuitikia kwa msaada unaotakiwa bila kuombwa.
Mwitikio wo wote unaotoa, iwe ni muda, rasilimali, kipawa, au neno la kutia moyo, ni tendo la kutumika. Lakini pia Mungu anafahamu kwamba uwezo wetu una kikomo katika yale tunayoweza kusaidia, kwa hiyo anatarajia kwamba tutaonyesha kuwajibika na uwakili mwema tunapohusika na jambo.
Shauku ya Mungu ni sisi kujitoa kwa furaha. Wakati mwingine ni vigumu kwa baadhi yetu kusema hapana, ukweli ni kwamba kujitoa kupita uwezo kunaweza kuondoa changamko na furaha ambayo Mungu hutaka tuwe nayo tunapotumika.
Kuhusu Mpango huu
Maisha yenye kusudi na yaliyojaa furaha, hujengwa kwenye mahusiano, upendo na imani. Kama unataka njia iliyonyooka zaidi ya mpango wa Mungu kwa maisha yako, tumia mpango huu kukusaidia kuweka mkazo katika hilo lengo lako. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2