Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi!Mfano
“Kuwapenda Wengine”
Kunapokuwepo hali ya kushamiri na kukua katika kumpenda Mungu katika maisha yetu, uwezo wetu wa kuwapenda wengine nao pia huongezeka vizuri. Kunapokuwepo upendo uliokomaa wa kuwapenda wengine kunakuja ile shauku inayokua ya kuonyesha huo upendo, hivyo kutimiza moja ya kusudi la muhimu la Mungu kutuumba – kutenda mema kwa wengine.
Ni katika mpango wa Mungu kwamba wakati wote tuonyeshe upendo kwa vitendo. Kila mmoja wetu yu katika mpango mkuu wa Mungu kugusa maisha ya watu wengine kupitia matendo mema.
Kila wakati tunapogusa maisha ya mtu mwingine kupitia neno jema, kufikia hitaji fulani, au kuwa msikivu kwa moyo ulioumia, sio tu kwamba tunaonyesha upendo wetu, lakini pia upendo wa Mungu kwao kupitia sisi. Kwa jinsi hii tunakuwa vyombo muhimu vya kung’arisha utukufu wa Mungu kwa ulimwengu uliojaa giza na kukosa tumaini.
Kuangaza nuru yetu hasa ni kuruhusu nuru ya Mungu kung’ara kupitia sisi. Kuna njia tatu muhimu za kuangaza nuru ya Mungu kwa wengine:
1. Uwe mshuhudiaji mwenye ufanisi;
2. Watumikie wengine;
3. Ibada na Wakristo.
Kuweka imani yetu katika matendo katika njia hizi tatu huwawezesha wengine kuuona upendo wa Mungu, neema na rehema, yote kwa utukufu Wake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Maisha yenye kusudi na yaliyojaa furaha, hujengwa kwenye mahusiano, upendo na imani. Kama unataka njia iliyonyooka zaidi ya mpango wa Mungu kwa maisha yako, tumia mpango huu kukusaidia kuweka mkazo katika hilo lengo lako. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2