Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi!Mfano

“Kukuza Upendo Wetu kwa Mungu”
Kukuza upendo kwa Mungu inawezekana ikawa ni vigumu zaidi kuliko kuongeza upendo na rafiki au mwanafamilia. Moja ya sababu za msingi ni kwamba hatuwezi kumuona uso kwa uso Mungu. Kwa hiyo inahitaji imani kudumu na kuongeza upendo kwa Mungu.
Imani inatuwezesha kuwa na upendo wa kweli kutoka mioyoni mwetu kwenda moja kwa moja kwa Mungu, hata kama hatumuoni na macho yetu ya nyama. Ili kukuza upendo wetu kwa Mungu, imani lazima iwe hai katika maisha yetu ya Kikristo.
Tunaposoma Neno la Mungu, kujali upendo Wake na ku-uhusisha katika maisha yetu na wengine, na kumwabudu kwa maombi, tunaaanza kumjua Mungu zaidi na zaidi. Kumjua zaidi baada ya muda inajenga upendo usio na unafiki unaokua kwake Yeye katika maisha yetu.
Kukuza upendo huo kwa Mungu kutoka katika imani yetu pia inategemea na kuonyesha upendo huo kwa matendo. Upendo wetu kwa Mungu kupitia imani, ukiambatana na kujitoa kwetu kwa Mungu kupitia matendo yetu ndio ufunguo unaohitajika kwa mawasiliano yanayokua na yenye mafanikio na Yeye.
Wakati upendo wetu kwa Mungu unapokuwa na uhakika wa kukua kutokana na kuweka imani yetu katika matendo, ni muhimu pia kufahamu kuwa hayo matendo yetu sio kwamba ndio sababu ya sisi kupata upendo na kibali cha Mungu.
Ukweli ni kwamba Mungu tayari alitupenda sisi sana na bila sababu yo yote hata kabla hatujamjua Yeye. Upendo wa Mungu ndio kiini cha upendo wetu: upendo wetu kwake na kwa wengine.
Kuhusu Mpango huu

Maisha yenye kusudi na yaliyojaa furaha, hujengwa kwenye mahusiano, upendo na imani. Kama unataka njia iliyonyooka zaidi ya mpango wa Mungu kwa maisha yako, tumia mpango huu kukusaidia kuweka mkazo katika hilo lengo lako. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2