Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi!Mfano
“Uwe Mshuhudiaji Mwenye Ufanisi”
Kujua jinsi ya kuwa mshuhudiaji mwenye ufanisi katika ulimwengu wetu wa kila siku huanzia kwa kufahamu Mungu anataka wengine waone nini katika maisha yetu. Jibu fupi ni, Yesu. Lakini hiyo ina maana gani?
Yesu anatoa mfano kamili wa jinsi Mungu anavyotaka sisi tuishi. Ingawa Yesu aliishi maisha yake ya duniani katika ulimwengu uliokuwa tofauti sana na wetu leo hii, Alionyesha tabia kamilifu ya Mungu na anatoa kielelezo sahihi kwa ulimwengu wetu wa leo.
Ni tabia ya Mungu ambayo anataka aikuze katika maisha yetu na ionekane na wengine. Hili linafanikiwa kupitia uhusiano wetu binafsi na Yesu tu.
Kama tawi linalobaki limeunganishwa katika mzabibu unaolipa uhai wake linavyozaa matunda, ndivyo ilivyo kwetu tunaobaki na uhusiano wetu na Yesu – tunazaa matunda – au kuonyesha tabia za Mungu kupitia maisha yetu kwa wengine.
Tabia ya Mungu inapofanya kazi ndani yetu na kupitia sisi – Upendo wake, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, wema,uaminifu, upole na kiasi tunakuwa washuhudiaji wenye ufanisi kwa kuishi maisha yetu ya kila siku.
Kama ilivyokuwa siku za Yesu, ile hali ya nje, mwonekano ulio hai wa tabia ya Mungu kupitia maisha yetu – tunda la Roho – unaonekana wazi. Unawavuta wote, waamini na wasioamini, ni jambo ambalo kila mtu analihitaji.
Jiandae. Mtu fulani anaweza kuwa anakuangalia na kuulizia juu yako bila wewe kutazamia. Ushuhuda wako binafsi wa wokovu na wa kazi ya ajabu ya Mungu katika maisha yako ni mahali pakuu pa kuanzia. Wakaribishe kanisani unaposali au mahali mnapofanya ibada, na watie moyo wanapotafuta uhusiano na Mungu!
Kuhusu Mpango huu
Maisha yenye kusudi na yaliyojaa furaha, hujengwa kwenye mahusiano, upendo na imani. Kama unataka njia iliyonyooka zaidi ya mpango wa Mungu kwa maisha yako, tumia mpango huu kukusaidia kuweka mkazo katika hilo lengo lako. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2