Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 2 YA 30

Andiko la Injili ya Yohana iliandikwa baada yaPetro kuuawa! Petro alikuwa mfia dini. Aliuawa miaka 32 hivi baada ya Yesu kupaa Mbinguni. Simulizi moja la historia ya kanisa lasema kwamba alisulibishwa miguu ikiwa juu na kichwa chini! Rudia m.18-19: Yesu akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka.
Akasema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate. Petro alimfuata Yesu na kumkiri mpaka dakika ya mwisho! Hivyo alifanikiwa kutimiza ahadi ambayo mara ya kwanza alishindwa: Mimi nitautoa uhai wangu kwa ajili yako(Yn 13:37)! Unamjibuje Yesu akikuuliza: Wewe wanipenda kuliko hawa(m.15)?

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz

Mipango inayo husiana