Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 4 YA 30

Musa anaelekea kufa. Hivyo kuanzia sasa BWANA ataongea na Yoshua moja kwa moja. Ili Yoshua asaidiwe kuamini jambo hili, Mungu anajitokeza kwenye nguzu ya wingu lile lile ambalo lilikuwa linathibitisha kuwepo kwake katikati ya taifa la Israeli tangu waondoke Misri (m.14-15: Bwana akamwambia Musa, Tazama, siku zako za kufa zinakaribia, umwite Yoshua, nanyi mkajihudhurishe katika hema ya kukutania, ili nipate kumwagiza kazi. Musa na Yoshua wakaenda, wakajihudhurisha ndani ya hema ya kukutania. Bwana akaonekana katika Hema katika nguzo ya wingu; na ile nguzo ya wingu ikasimama juu ya mlango wa Hema). Bwana anafahamu kwamba baadaye Waisraeli watamwacha yeye na kuigeukia miungu (m.20: Waisraeli watakapokwisha kula na kushiba, na kuwanda; ndipo watakapoigeukia hiyo miungu mingine, na kuitumikia, na kunidharau mimi, na kulivunja agano langu). Bila shaka alikuwa anaumia sana akikumbuka anavyoshughulika kwa ajili yao. Hata hiyo anamwahidi Yoshua, Nami nitakuwa pamoja nawe(m.23).

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz

Mipango inayo husiana