SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano
Pale mlimani Sinai, Mungu amefanya agano na wana wa Israeli, nao wamekuwa watu wa Mungu. Wapo safarini, wakisafiri pamoja na Mungu kila siku. Hata imekuwa kana kwamba hii safari yao ni ya Mungu pia. Daima wanapokea maelekezo ya safari kutoka kwa Mungu. Matendo yao safarini ndiyo yanayowapa baraka pale walipo na kule waendako. Safari yao ilikuwa ya kufuata agano lao na kutwaliwa na damu ya agano. Rudia m.8 unaosema, Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote. Habari hii muhimu inafafanuliwa ifuatavyo katika Waraka kwa Waebrania: Kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote, akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu(Ebr 9:19-20). Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu, awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina(Ebr 13:20-21). Kwenye msingi huu, Petro anawaandikia Wakristo:Mungu Baba alitangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu(1 Pet 1:2). Wewe je, unasafirije katika safari yako kwenda mbinguni? Umetwaliwa na damu ya Agano Jipya?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz