Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano
Yesu anafundisha juu ya usafi wa kiroho. Katika hili Mafarisayo na waandishi walikwenda kinyume cha ukweli wa Mungu kwa njia mbili: 1.Waliyahesabu mafafanuzi ya sheria za Mungu (hayo yanayoitwa mapokeo yaokatika m.3) kuwa muhimu kuliko sheria zenyewe za Mungu. Hivyo walilitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yao (rudia anavyosema Yesu katika m.3-6!) Nasi tulipokee fundisho hili. Tusiwe tunahesabu mafafanuzi yetu ya Neno la Mungu (theolojia yetu) kuwa sawa na, au juu ya Neno la Mungu! 2.Walikuwa wanaangalia usafi wa nje tu. Lakini huo hautoshi kwa Mungu. Zingatia Yesu anavyoupima katika m.8, akinukuu ilivyoandikwa katika kitabu cha Isaya, Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami. Vilevile katika m.18-20 Yesu anasema, Vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano; hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi. Hivyo bila Mwokozi tutapotea!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz