Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

SIKU 13 YA 31

Ezekieli aliishi kati ya wafungwa wa Yuda katika ukingo wa mto Kebari, nchini Babeli. Mungu alimwita awe nabii wao. Wito ulimjia Ezekieli mwaka 593 KK mbingu zilipofunuka (m.1). Alipotazama kwa mshangao mabadiliko ya rangi angani yaliyotokana na radi katika wingu jeusi, alipata maono. Anaona viumbe hai vinne. Katika 10:2 anaambiwa ni makerubi, yaani, aina fulani ya malaika: Ingia kati ya magurudumu yazungukayo, yaani, chini ya kerubi, ukaijaze mikono yako yote miwili makaa ya moto, toka katikati ya makerubi. Jambo kuu la viumbe hivi si sura yao, bali kwamba walikwenda moja kwa moja Roho wa Mungu alikotaka kwenda (m.12, Walikwenda kuelekea mbele, kila mmoja wao; roho ilikotaka kwenda ndiko walikokwenda; hawakugeuka walipokwenda).

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz