Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

SIKU 17 YA 31

Kama vile mlinzi awaonyavyo wenyeji wa mji akiwaona maadui wanaotaka kushambulia, ndivyo Ezekieli alivyopaswa kuwaonya Waisraeli waliokuwa kifungoni. Waache dhambi zao na kuokolewa ili wasipate maafa zaidi ya yale waliyokwisha yapata. Iwapo Ezekieli angewaonya watu, nao wangedharau onyo lake, hao wangechukua lawama juu ya maafa yao. Lakini kama angeacha kutoa onyo, yeye angedaiwa kutoa hesabu kwa vifo vya watu hao. Basi, Ezekieli awaonye, nao wakubali onyo la Mungu, ili wapone wote.

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz