Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

SIKU 20 YA 31

Tangu Mungu alipowatoa Waisraeli utumwani Misri, aliwafundisha tena na tena kuwa hakuna Mungu ila Yeye, na wasiabudu miungu (Kut 20:1-5, Mungu akanena maneno haya yote akasema,Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.Usiwe na miungu mingine ila mimi.Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao). Lakini miungu ilinasa maisha ya wateule wake. Leo tunaona ibada za miungu katika mitindo mipana zaidi. Watu wanaabudu fedha, mali, uzinzi na anasa kuliko kumwabudu Mungu. Somo la leo litufundishe kuwa Mungu akituonya, hasemi bure. Atawaacha wachache wabaki hai (m.8: Nitasaza mabaki; maana mtakuwa na baadhi ya watu watakaoukimbia upanga kati ya mataifa, mtakapokuwa mmetawanyika katika nchi za watu.Angalia vilevile neno hili “chache” katika 5:3 ambapo nabii anaambiwa,Twaa nywele chache katika hizo). Mungu atawaacha wachache ili washuhudie ukweli huu na kujichukia kwa sababu ya mabaya hayo waliyotenda.

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz