Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

SIKU 19 YA 31

Huu ndio Yerusalemu, anaeleza Mungu kuhusu tendo la kimfano katika m.1-4. Je, ni sisi pia? Tunaonywa katika mafundisho mengi kwamba Mungu anachukia uasi, tena atauadhibu. Lakini tumesikia na kusahau. Hivyo tunaelekea kuasi kuliko wasioamini (linganisha na ilivyoandikwa kuhusu mji wa Yerusalemu katika m.6, Umeasi hukumu zangu, kwa kutenda mabaya kuliko mataifa hayo, nao umeasi sheria kuliko nchi hizo ziuzungukazo; maana wamezikataa hukumu zangu, wala hawakuenda katika sheria zangu). M.9 unaogopesha, Mungu akisema, Nitakutenda nisiyoyatenda zamani, wala sitafanya tena mambo kama hayo, kwa sababu ya machukizo yako yote. Mungu ataadhibu kwa kiwango asichowahi kutenda, na pia hatatenda tena hivyo. Ni hatari kuzoea kutenda dhambi, kwa sababu matokeo yake ni hukumu. Tuepuke hali hii, tukiomba Mungu atupe sikio la kusikia kama watu wafundishwao.

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz