Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 21 YA 31

Mfalme wako anakuja kwako … naye ana wokovu (m.9). Wayahudi washangilie na kufurahia habari hii njema. Ujio wa huyo ni tofauti na ule wa wafalme wengine wote wa dunia hii. Si mfalme wa vita. Amepanda punda kuonesha kuwa ni Bwana wa amani, mpole na mnyenyekevu. Ataleta amani kwa mataifa yote. Tufurahi na sisi, maana ndivyo Yesu alivyoingia mji wa Yerusalemu kama Masihi na Mwokozi akiwa tayari kwenda msalabani. Angalia ni damu yake ya agano inayotufungulia kuwa huru na wenye amani, kama ilivyoandikwa katika m.11, Kwa habari zako wewe, kwa sababu ya damu ya agano lako, nimewatoa wafungwa wako katika shimo lile lisilo na maji!

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/