Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 23 YA 31

Ndiye Bwana aletaye nafaka na divai: Nafaka itawasitawisha vijana wanaume, Na divai mpya vijana wanawake (9:17b). Kwa hiyo Waisraeli walijua kuwa wamtegemee Bwana awape mvua wakati wake. Lakini inaonekana taifa lilikosa uongozi thabiti wa kiroho. Watu wakaanza kutumaini ibada za miungu ili kupata mafanikio. Kwa hiyo hasira ya Bwana iko juu ya viongozi hao walioacha kuwaongoza watu katika kweli yake. Anaahidi kuwaondoa. Wakati uleule atawatia wadhaifu nguvu kubwa, hao wawe chombo chake cha kufaa. Je, wewe unao msimamo upi juu ya changamoto hii?

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/