Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano
Katika Zek 11 Waisraeli walimkataa mchungaji wao mwema. Lakini Bwana atakapowamwagia Roho wake, watajuta. Watatambua kwamba ushindi wao watoka kwa Bwana tu, na umepatikana kwa gharama aliyoilipia Masihi waliyemkataa. Watamtazama yeye ambaye walimchoma ni unabii juu ya kifo cha Yesu, Mwana pekee wa Mungu. Katika Yn 19:33-37 tunasoma ilivyotokea, Askari walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji. Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda wake ni kweli; naye anajua ya kuwa anasema kweli ili ninyi nanyi mpate kusadiki. Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na tena andiko lingine lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma. Yaonesha kwamba sasa wanamwamini, wakimwomba awaokoe kwa neema yake. Wanafanya maombolezo kila mmoja peke yake, siyo kwa ujumla. Ndivyo ilivyo hata sasa kwa kila anayetubu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/