Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 30 YA 31

Ukombozi utaletwa ghafla, tulisoma jana. Somo la leo laeleza itakavyowezekana. Wote waliofanya vita juu ya Yerusalemu watakufa kwa tauni ya pekee, maana inaelezwa zaidi kama mashaka makubwa yatokayo kwa Bwana (m.13). Ndiye Bwana atakayeingilia kati. Kwa hiyo utukufu wa Bwana utakuwepo tena, si katika mji wa Yerusalemu tu, lakini katika nchi nzima pia. Nchi hiyo itasawazishwa ili nyumba ya Mungu ionekane pande zote. Ni ahadi katika Zek 2:4 na Isa 2:2 zinazotimia. Tafakari ahadi hizo! Piga mbio, kamwambie kijana huyu, na kusema, Yerusalemu utakaliwa na watu, kama vijiji visivyo na kuta, kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo ndani yake. ... Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.

siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/