Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 20 YA 31

Watu wengi wa mataifa watajiunga na Israeli, kama unabii katika 8:23 unavyosema, Bwana wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi. Lakini siyo wote watakaojiunga. Kwa hiyo twasoma sasa jinsi Mungu atakavyohukumu mataifa ya jirani kwa sababu ya kiburi chao, kama anavyosema katika m.6, Mwana wa haramu atatawala huko Ashdodi, nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti. Hao waliotesa Israeli watakapoadhibiwa, italeta hali mpya kwa watu wa Mungu. Mwenyewe atakuwa ulinzi wao, na mtu awaoneaye hatapatikana tena kwao (m.8, Nami nitapiga kambi yangu pande zote za nyumba yangu ili kuwapinga adui, mtu awaye yote asipite ndani yake wala kurudi; wala mtu aoneaye hatapita tena kati yao; kwa maana sasa nimeona kwa macho yangu). Hivyo Mungu hataruhusu watu wake waangamizwe kabisa, kama vile Yesu alivyosema kuhusu Kanisa kwamba milango ya kuzimu haitalishinda (Mt 16:18).

Andiko

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/