Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 19 YA 31

Hukumu ya Mungu katika m.11 inasema, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako. Tunaona inatimia. Kupitia nabii Ahiya, anamwahidi Yeroboamu, mtumishi wa Sulemani, utawala juu ya sehemu kubwa ya Israeli. Hii itufundishe kuwa bila ulinzi wa Mungu hata tunaowaamini wanaweza kutugeuka. Hivyo kukatokea uhasama baina ya Sulemani na Yeroboamu, hata ikamlazimu Yeroboamu kukimbilia Misri ambako alijua angesaidiwa kutwaa utawala. Nafasi yake ilitokea Sulemani alipokufa baada ya kuongoza kwa miaka arobaini. Lakini Yeroboamu hakukubali shauri la kumtii Mungu.

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/