Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 18 YA 31

Kuasi kwa Sulemani kulifanya ulinzi wa Mungu uondoke juu ya uongozi wake. Matokeo yake, wafalme wa nchi za jirani wakajipanga na wakafanikiwa kuudhoofisha utawala wa Sulemani. Tujifundishe kuwa mtu anapoasi, ulinzi wa Mungu hautabaki kwake. Atakamatwa na kuwa chini ya uongozi wa shetani. Kibaya zaidi, ikiwa ni kiongozi anayeasi, anahatarisha hata watu anaowaongoza. Hebu fikiri mtawala anaporuhusu vita, jinsi ambavyo wananchi wanataabika. Tusiache kuwaombea viongozi wetu watende yaliyo mema.

siku 17siku 19

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/