Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Baada ya fimbo ya Haruni kugeuzwa kuwa nyoka, pia wachawi wa Misri waligeuza fimbo zao kuwa nyoka (ling. m.10,Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka; na m.12,Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka). Ila nyoka hao walimezwa na nyoka wa Haruni. Hata hivyo, Farao aliufanya moyo wake kuwa mgumu, kama BWANA alivyosema. Wamisri walipata taabu, kwani maji ya mito yao yote yaligeuzwa kuwa damu. Nidhahiri kwamba viongozi wasiposikiliza maagizo ya Mungu, watu wanapata shida, majira yote. Ni vizuri ujiulize: Je, ninafuata maagizo yote ya BWANA? Ni watu wangapi wanaoathirika kwa kutokuwa mtii?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/