Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

SIKU 7 YA 31

BWANA alimwagiza Musa kumwona Farao amsisitizie kutoa ruhusa kwa Waisraeli. Pigo aliloambiwa litapiga ni mvua ya mawe ambayo itaharibu kila kitu: mimea, wanyama, na watu. Farao aliambiwa amekuwa kiongozi kwa kusudi kubwa la Mungu kujitukuza kupitia yeye. Ndiyo maana Mungu akasema,Wakati huu ningekwisha kuunyosha mkono wangu, na kukupiga wewe na watu wako, kwa tauni, nawe ungekatiliwa mbali na kuondolewa katika nchi; lakini, nilikusimamisha wewe kwa sababu hii hii, ili nikuonyeshe uweza wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote(m.15-16). Matokeo yake yaliharibu kama neno la BWANA lilivyosema,Mvua ya mawe ikapiga kila kilichokuwako mashambani, binadamu na mnyama, katika nchi yote ya Misri; hiyo mvua ya mawe ikapiga kila mmea wa mashambani, na kuuvunja kila mti wa mashamba (m.25).Katika pigo hili, watu wa Mungu walilindwa, wasipate madhara yoyote. Yaanikatika nchi ya Gosheni peke yake, walikokaa wana wa Israeli, haikuwako mvua ya mawe(m.26). Mungu hashindwi kukuwekea wigo ukalindwa na hatari zinazowapata wasiomjua Mungu. Zingatia ahadi hii ya Bwana:Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele(Zab 121:7-8).

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/