Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

SIKU 12 YA 31

Mungu anatoa maelekezo kuhusu kutoka Misri: 1) Watachinja mwanakondoo aliye mkamilifu. Anasema,Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi(m.5). 2) Watapaka damu yake kwenye milango kuwa ishara kwa BWANA atakapopita:Ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri(m.13). 3) Watamla kondoo aliyechomwa na mkate usiotiwa chachu. 4) Watakula kwa haraka, wakiwa wamejiandaa kusafiri:Mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana(m.11). Tena watahesabu tukio hili kuwa mwanzo wa maisha yao kama watu wake (ling. m.2,Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu). Kristo aliyefanywa kondoo wa pasaka ni utimilifu wa pasaka. Damu yake ilimwagika msalabani ili tukombolewe.

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/