Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Hatimaye Farao anawaruhusu Waisraeli kutoka Misri. BWANA alipiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri (watu na wanyama). Kukawa na kilio kikali katika jamii yote. Farao aliwaita Musa na Haruni, akawaambia waondoke wakamtumikie BWANA. Hata anaomba yeye naye apate baraka:Twaeni kondoo zenu na ng'ombe zenu kama mlivyosema, enendeni zenu, mkanibariki mimi pia(m.32). Alisema hivyo, maana alitambua kwamba Mungu wa Waisraeli ni Mungu mkuu. Utisho wa BWANA ni juu ya Wamisri. Kwa hiyo wanawahimiza Waisraeli watoke kwa haraka, nao wakatoka kwa ushindi wakibeba nyara. Mungu wetu ni mkombozi kweli.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/