Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Edomu ni kizazi cha Esau na ndugu wa Israeli, kizazi cha Yakobo. Lakini Edomu hakujali uhusiano huo wa kinasaba, akampiga Israeli bila huruma. Mungu aliazimu kulipa kisasi. Waamoni kwa kutamani ardhi ya Waisraeli, waliwafanyia ukatili mkubwa wa kuwaua wajawazito na mimba zao. Nao Wamoabu kwa kutoheshimu masalia ya wafu, walimkasirisha Mungu ambaye atawaadhibu. Jumla ya yote ni kwamba watendao kwa udhalimu hawatadumu: “Uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya, aliondoe kumbukumbu lao duniani” (Zab 34:16).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/