Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Mungu anatamka kilio katika taifa lake la Israeli. Ni kilio kinachotokana na kipigo chake mwenyewe. Tangu kuchaguliwa kwake, Mungu aliita Israeli “bikira”, akimaanisha anataka awe mume wao wa kiroho, yaani Mungu wao pekee, na watembee katika usafi na upekee huo. Lakini Israeli walijichafua kwa kuiabudu miungu. Hapo Mungu aliudhika. Hata hivyo, pamoja na tangazo la maangamizi makubwa, analia katika maumivu ya upendo,Nitafuteni mimi, nanyi mtaishi(m.4). Katika m.6 anasisitiza jambo hili akirudia kuwaita,Mtafuteni Bwana, nanyi mtaishi. Leo mwaliko huu una maana gani kwako?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/