Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

SIKU 27 YA 31

Fungu hili la maneno linatupa mambo matatu aliyopata kuyaona Amosi kuhusu hukumu ya Mungu: Nzige, moto na timazi. Nabii alipowaombea watu wake, nzige na moto zilikoma. Naye akaendelea kuwaombea mpaka Mungu aliposema,Sitawahurumia tena(m.8 tafsiri ya NENO; timazi ni mfano wa kupima kama watu wana unyofu wa maisha). Mungu anatusihi maombezi yafanyike kwa ajili ya watu wote ili uwepo utulivu na amani nchini, nao waokolewe. Anasema,Kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli(1 Tim 2:1-4). Ni wajibu wa watu wateule kuombea taifa lao mambo hayo.

Andiko

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/