Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Mafanikio na ustawi wa kimwili ni vitu hatari kwa usalama wetu wa kiroho tusiporuhusu Mungu atunyenyekeshe. Katika ustawi twawaangalia wasio na mafanikio kwa dharau, wala si rahisi kuwa na chembe ya huruma. Kwa kuwa Mungu achukia mioyo hii ya kujiona na kujitukuza, mioyo isiyo na nafasi ya kuwaangalia wanyonge kwa huruma, ataachia hasira yake juu yetu. Kuna wito katika maneno haya unaotuamsha tusilale kwenye hariri ya ustawi wetu, bali tuwahurumie wanaohitaji na vitu hivyo tulivyopewa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/