Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

SIKU 30 YA 31

Macho ya Bwana MUNGU yanauangalia ufalme wenye dhambi, nami nitauangamiza utoke juu ya uso wa dunia(m.8). Kauli hii yaeleza kwa ufupi ujumbe mzima wa mistari hii tuliyosoma. Haiwezekani kujiepusha na hukumu ya Mungu. Ni kauli ya kutisha, na ni malipo halali kwa watenda dhambi. Mungu anasema,Wenye dhambi wote katika watu wangu watakufa kwa upanga, hao wasemao, Mabaya hayatatupata nyuma wala mbele(m.10). Tena ni kipimo halali kwa jeuri dhidi ya Mungu. Pia ni tahadhari ya mwisho kwetu tuliopendwa, lakini tukajiendea kwa njia za uhuru haramu. Neno laonya katika Ufu 2:5,Kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu.

siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/