Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Bwana Yesu alifundisha katika Lk 10:3 kuwa anawatuma wafuasi wake kati ya mbwa-mwitu. Akawaambia,Enendeni, angalieni, nawatuma kama wana kondoo kati ya mbwa-mwitu. Wenyewe watashambuliwa, na kazi yao itapuuzwa. Lakini Mungu anataka tuendelee kukemea dhambi na kuonesha njia ya haki siku zote. Katika Isayakuna mkazo huo huo kwamba Injili na kweli za Mungu zihubiriwe, lakini watu watakataa. Katika Isa 6:9-12 Isaya anajulisha Mungu alivyomwambia,Akaniambia, Enenda, ukawaambie watu hawa, Fulizeni kusikia, lakini msifahamu; fulizeni kutazama, lakini msione. Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito masikio yao, ukayafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa. Ndipo nilipouliza, Ee Bwana, hata lini? Naye akanijibu, Hata miji itakapokuwa ukiwa, haina wenyeji, na nyumba zitakapokuwa hazina watu, na nchi hii itakapokuwa ganjo kabisa; hata Bwana atakapowahamisha watu waende mbali sana, na mahame yatakapokuwa mengi ndani ya nchi. Hivyo Mungu atakuwa amehukumu kwa haki atakapohukumu. Amazia anataka kumzuia Amosi na kutetea uovu wa Yeroboamu, lakini bado Mungu atahukumu, maana ni mhukumu wa haki.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/