Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Hutokea Mungu anatufunulia makusudi yake kwa vielelezo kama hili kapu la matunda mabivu. Waisraeli wameiva tayari kuvunwa. Uvumilivu wa Mungu umefikia ukomo. Sasa kinachoendelea ni hukumu juu ya dhambi ya maonevu na dhuluma zilizofanywa na watajiri kujinufaisha isivyo haki. Zaidi ya mapigo dhahiri, Mungu ataacha kusema nao. Atazuia Neno lake. Yaliyokuwa yakitendwa na Israeli hutendeka kwetu kwa viwango vikubwa. Tumshukuru Mungu akinena nasi, na tumsikilize, tusije tukakosa neno lake kama hao.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/