Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Bwana atawarejeza tena watu wake. Maneno haya yanaashiria kurudi kwa wana wa Yuda katika nchi yao baada ya utumwa wa miaka 70 huko Babeli, na hata watu wa mataifa kuingia katika ufalme wa Mungu kipindi cha kanisa la kwanza.Baada ya mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha; Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana, Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao; Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele(Mdo 15:16-18). Mungu hana hasira milele. Katika Zab 103:9 twasoma,Yeye hatateta sikuzote, Wala hatashika hasira yake milele.Pia Mungu mwenyewe anasema,Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya(Isa 54:7). Hata sasa anaonesha uvumilivu wake kwa wenye dhambi, na yuko tayari kuwasamehe na kuwapokea tena kwake. Kama unahukumiwa moyoni kuwa mkosa, huu ni ujumbe mzuri kwako. Rudi kwa Bwana wako, atakurudia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/